December 12, 2011

Bunge halijakataa poshoHabari ya siku nzuri uliyoianza asuhuhi.  Kama watanzania wengine wenye bahati ya kukutana na magazeti, nimeamka na kupata nakala yangu ya gazeti pendwa The Citizen. Habari kubwa iliyopata macho yangu inasema: Wabunge wakataa posho, wasubiri uamuzi wa rais(Bunge stops allowances,looks out for JK decision).
Ni heading nzuri. Lakini nina kesi nayo. Ukisoma habari inasema kamati ya utumishi wa wabunge imesema ulipwaji wa posho mpya zilizopendekezwa utategemea maamuzi ya raisi. Kwa mtazamo wangu huko si kukataa posho.

Nachoweza kusema ni kuwa kamati ya bunge, imeeleza tu nini kinachofuata katika hatua za kawaida zinachokuliwa siku zote kabla ya kuongeza posho za vikao kwa wabunge. Kwa kweli hilo hata si jipya. Kumbuka katibu wa Bunge alisema jambo  hilo hilo, likatafsiriwa kwa haraka na baadhi ya wachambuzi na baadhi ya waandishi kuwa amesema posho hazijapandishwa. Nilimwelewa kuwa hakuna mbunge aliyelipwa posho mpya.

Kisha Makinda, spika wa bunge akasema kwa kusisitiza, kwanini wameamua kupandisha posho. Lakini pia hakusema kama posho zimelipwa. Kwa uwazi sana alisema anaunga mkono kupandishwa kwa posho. Na hiii ilivuta usikivu wa watu kwa mshangao. Namna gani maisha yawe magumu kwa wabunge tu hapo Dodoma?

Nilimsikiliza vizuri Makinda akisema wameamua kupandisha maslahi ya wabunge, na mahali walipoona ni rahisi kufanya hivyo ni kupitia posho za vikao kwa kuwa hizo zinahitaji tu mapendekezo yao na kisha ukubali wa raisi. Mishahara ingekuchua mlolongo mrefu zaidi.

The Citizen linanukuu vyanzo vya habari toka kamati ya huduma za bunge wakisema kuwa mapendekezo yamewasilishwa kwa raisi. Hiyo si kukataa posho. Wangekuwa wamekataa wangetangaza kuwa wameondoa mapendekezo yao kwa raisi, hawataki tena kujaribu kuongeza posho.

Napendekeza The Citizen ingesema kuwa suala kuongeza posho za wabunge limefika/ameachiwa Rais Kikwete. Kisha wangemtafuta Makinda aseme kwanini aliongea kauli iliyoonekana kuzidi mamlaka yake. Kama ni rais ndiye anaidhinisha, basi yeye kama spika hakutakiwa kusema wameongeza, angesema wamependekeza.

Kuna mengine nahitaji kuongelea kuhusu hili swala. Kwa namna lilivyojitokeza kwenye vyombo vya habari na namna lilivyoongelewa na wasemaji tofauti tofauti: Spika. Katibu Mwenezi wa CCM, Wabunge wa Upinzani, Wanafunzi wa Vyuo, Chama cha Waalimu na wengineo. Nitakuja kuongeza baadaye kwenye makala hii. 

No comments:

Post a Comment